Kila uchao nimeishia tu kuwaza Kwa mengi na machache najikwaza Japo ni hali ngumu moyo unakataza Lakini bado naamini penzi umelijaza Na ndio maana kila uchao najikaza Labda ipo siku ambayo utaniliwaza Si ati uje na makavu ya kunicharaza Najua unataka softlife, nitakutandaza Na hapa kwangu lazima nitakupangaza Kwa hali zote, yaani giza kwa mwangaza Kwa shida na raha, mifukoyo nitajaza Kwa nyama na mifupa, moyo utapakaza Kwa mengi na machache, kifuani nitakulaza Kwa mafupi na marefu, maisha tayasongeza Maana wewe ndio wangu, lazima nitajikaza. |C-Cece| Maisha pamoja ni shwari Umenifunza kuwa hodari Kila unapotaka niwe hatari